1 Chronicles 22:14-16

14 a“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,000
Talanta 100,000 za dhahabu ni sawa na tani 3,750.
za dhahabu, talanta 1,000,000
Talanta 1,000,000 za fedha ni sawa na tani 37,500.
za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza.
15Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”

Copyright information for SwhKC